Vitu vinavyosababisha adui ‘UJINGA’ kutawala Watanzania wengi

Na Deogratius Kilawe

1. Kazi za magazeti ya udaku na mengine yasiyokuwa makini

BAADHI ya taarifa katika vyombo vyetu vya habari huwa hazina umakini lakini utafiti unaonyesha kwamba asilimia 80% ya Watanzania wakiwamo wasomi ndizo taarifa kwao wanazozipendelea.

Taarifa hizo kwa maoni yangu kuishia kupanda mbegu ya ujinga na hivyo kupelekea kila wiki kuvuna  wajinga  wengi sana.

Vile vile baadhi ya taarifa huwa zinaandaliwa kwa hisia  za mwandishi kuwa  ndio tukio  na hali halisi (facts) na kupewa uzito wa juu na kukuta Watanzania hao kuishia kuvuna mawazo ya mtu (mwandishi).

Athari za taarifa hizo ni  kuwa na watu wasio na uwezo wa kuchangia mada au ajenda kwa kuwa wana taarifa za watu walizojaza kichwani na sio mada/ajenda hivyo ukiwaleta katika mada ni weupe.

2. Exposure (kutoka nje ya nchi)
Nchi yetu ni ya uchumi huru lakini watu kiukweli bado tupo tuna fanya  na kuishi maisha ya uchumi usio huru (closed economy) watanzania karibia wote waliotoka nje ndio ambao wenye upeo wa mambo ya kimaendeleo na ndio wanaojitahidi kuingia katika katika soko la dunia lakini ni wachache sana.

Tujiulize je kama tunataka kuendelea wakati wanafunzi wanaofanya exchange program nje ya nchi ni wachache, wanaoenda kusoma ni wachache, kufanya kazi bado ni wachache je tutawezaje kuendele kutoka hapa tulipo? Muda sasa umefika kuanza kupeleka ndugu zetu nje ya nchi kwa wingi wakaitangaze  na kuleta teknolojia mpya na mawazo tofauti na kusababisha kuwa na taifa la wajanja.

Inasemekana nchini Nigeria karibia kila raia wa Nigeria ni mjanja hakuna wa kumdanganya.

3. Kutokuwa na muda wakufikiri kila siku;
Tanzania maeneo ya wazi kwa umma ya kumpuzika  ni madogo na machache sana mjini jua kali wiki nzima watu wapo resi na maisha yao  litakalo tokea kesho au baadae na liwe, watu wengi ni waathirika wa brain drain,muda  wa kufikiri hakuna na kama kama hujafikiri leo kesho kuna mtu atakufikiria na kukutawala.

Sasa nini tufanye kwa hili;
Tutenge maeneo mengi ya wazi kwa mapumziko kwa Watanzania,elimu kupitia media juu ya umuhimu wa kufikiri tukumbuke kama hatufirii leo kesho mtu atafikiria na kukutawala.

4. Kusoma vitabu;
Kuna msemo wa siku nyingi unasema kama unataka kumficha Mwafrika basi weka ujumbe kwenye kitabu.

Mara zote kama uantaka ukombozi wa kimaarifa basi huna budi kujifunza kutoka kwa wengine na wewe pia ujue nini ufanye ili ulete mabadiliko tofauti. Kuna aina tofauti za vitabu kwa watu wa dini vitabu vyao vitakatifu bado  hata theluthi hawafikia walio wengi. Muda sasa umefika acha kupenda kusikiliza anza sasa kusoma mwenyewe ili uwe huru,nunua vitabu na vipo vya kukusaidia wewe ufanikiwe kifedha, furaha, siasa, historia za mashujaa mbalimbali, mara ya kwanza utaona kawaida lakini kadri unavyozidi kuendelea kusoma vitabu ndio yanakuwa maisha yako  ya kila siku na kuwa sawa na kuamka mara ya pili.

5. Mfumo wa elimu na sera;
Mfumo wetu  unahitaji mabadiliko sana katika hii dunia ya utandawazi,ndio kuna dunia ziliendelea kwa lugha zao lakini mimi sina maana tukitupe Kiswahili bali ni kama tuna cheza mchezo wa makusudi wa kutengeneza matabaka  katika jamii.

Mfumo unahitaji kubadilika  mfano masomo yote yanatakiwa kufundishwa kwa kiingiingereza kuanzia chekechea, primary na kuendelea maana huwezi kumfundisha mtu Kiingereza na wote wakajua Kiingereza wakati umri wa wao (kipindi mototo ubongo wake una elewa zaidi sana umepita yaani kakomaa tayari)ni sawa na mafunzo ya sarakasi kama hukufanya ukiwa mdogo viungo bado havijakomaa  ukija ukubwani kama ukifanikiwa itakuwa kwa shida sana. Dunia kote, mfano China, Japan, na Urusi, kote huku sasa watu wanasoma kwa bidii.

6. Meditation;
Meditation ni muhimu sana kwa taifa kama hili,kwa maendeleo yaliyo bora na kuwa huru meditation inahitajika. Mara nyingi tunapata stress tutokapo kazini, tuna hitaji meditation ili kuondokana na haya yote na pia kupooza akili zetu zianze upya na kuwa na fikra pevu.

Mwandishi Deogratius Kilawe ni mfanyabiashara wa Dar es Salaam na mshauri binafsi wa masuala ya biashara.
Anapatikana kwa simu 0717109362
Email: deogratiuskilawe@yahoo.com

tushirikishane
 • Show Comments

 • Babu Jinga

  Hongera kwa Kuweka Mchango wako katika jitihada za kuwaamsha Watanzania ambao wengi wanazidi kubweteka na Kudhani jukumu la Ukombozi wao kifkra na kimaendeleo liko mikononi mwa Watu fulani km Wanasiasa,wafanya biashara ama wengine wote waliotambua udhaifu huo na kuutumia kujifanya wao ndio suluhisho la kutukwamua kwenye lindi hili la unyonyaji mpya Ukombozi wa kila mmoja huanzia malangoni mwake na siyo kwa mwingine. hawa wote wanasiasa na wengineo wanatumia uzuzu wetu kujinufaisha wao ndio maana hata wabunge wetu wanajiongeza posho bila kumjali mwananchi wa chini ambaye sasa anauziwa sukari kwa 2,000/= na mafuta ya taa 2,250/= mbona hawasemi mishahara ya kima cha chini ipande angalau hata kwa 100,000/= kwa vile maisha yamepanda kwa woye? wake up Tanzania and wake up the Tanzanian.Tusiwaendekeze wanasiasa wanaotupelka kwa falsafa ya ordo ab chao ili sisi tunapofanyiana vurugu na kupoteza muda wa kuzalisha wao wanajiimarisha kisiasa na kiuchumi

  • mweta loti

   mfumo wa lugha hasa ya kufundishia ni tatizo kubwa mno hatuwezi kufikiri kwa kiswahili na kuongea kwa kiingereza

 • simba

  Hello ndugu mwandishi, nashukuru sana kuona ulicho kiandika nichaukweli kabisa, mimi nipo naishi hapa Swiss sasa na miaka 5 naishi hapa sio kwa kusoma naishi hapa kama mwanach huru wa dunia, ni kweli kabisa vijana tunatakiwa kutoka na kuosha macho kufuta ujinga.

  Tanzania tumejaliwa na neema nyingi huwezi kuamini mpaka utoke uone hao waNageria ni wajinga huwezi kuamini kwa mimi navyo waona hapa wanavyo ishi. ni kweli habari ni nyenzo kubwa sana ya kuwafanya watu kujisahau na kujiona kuwa hatuwezi mpaka watu kutoka Ulaya waje huko kusaidia, vyombo vyetu vya habari vimejaa uchafu na upumbavu mtupu unawafanya watanzania wote kuwa wajinga, ni magazeti, na tv zetu hazifundishi chochote ni umbea na matatizo tu ndio vimejaa, nachoomba nduguzangu wote huko acheni kujisahau na kuona watu kutoka ulaya ndio wanaweza hata huko pia mnaweza tu, cha kufanya ni kuwa wabunifu na kuangalia dunia jinsi inapo kwenda kwani, mnacho kiona ktk TV na magazeti na facebook sio dunia hiyo, tutarudi huko na kuchukua nafasizenu mkibaki mna lalamika tu, watu wa kutoka nje, fungueni macho vijana wenzangu, wenu ktk ujenzi wa taifa

  SIMBA

 • harrid

  dah , yaani kaka kilawe hapo umenena, yaani sina cha kuongeza hata wachangiaji pia. nategemea kuichukua hii na kuituma kwenye facebuku manake wakati flani nahisi ipo haja ya kutumia right channel ili ujumbe umfikie mlengwa pale halipo. nimestaajabu pia uliposema kuna haja ya kutumia meditation.

Your email address will not be published. Required fields are marked *

comment *

 • name *

 • email *

 • website *

Sponsors

tushirikishane

You May Also Like

Waziri Mpango asisitiza uchumi umeimarika, aitaka sekta binafsi kushirikiana na serikali

Wakati mjadala ukiendelea juu ya hali ya uchumi nchini, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. ...

Sababu za wanajeshi wa Tanzania kuendelea kulinda amani nchini Congo DRC

Inaelezwa kuwa vikosi vya jeshi la Tanzania kuendelea kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ...

Zahanati yafungwa baada ya Muuguzi wake kwenda likizo!

WAKATI baadhi ya hospitali zikiathiriwa na mgomo wa madaktari, mkoani Mwanza kumetokea kituko baada ...