Kansa ya matiti ni miongoni mwa magonjwa yanayowatesa wanawake wengi duniani na kuhatarisha afya zao. Lakini kumekuwepo na hisia tofauti juu ya maumivu ya kawaida ambayo mwanamke anaweza kuyapata kwenye matiti yake.

Baadhi yao wamekuwa wakihusianisha moja kwa moja na kansa ya matiti. Maumivu ya matiti yanaweza kuwa ni sababu mojawapo ya dalili ya kansa lakini sehemu kubwa ya maumivu hayo ni matokeo ya madadiliko anayoyopata mwanamke katika ukuaji wake.

Kwa nini unasikia Maumivu ya Matiti?

 Wataalamu wa afya ya mama wanasema uwezekano wa maumivu ya matiti kuwa kansa ya matiti ni mdogo.

“Maumivu ya matiti peke yake kwa sehemu ndogo yanahusishwa na kansa”, anasema Dkt. Monique Swain wa Kitengo cha Matiti katika hospitali ya Henry Ford System iliyopo Detroit nchini Marekani.

Daktari Monique ambaye alikuwa akihojiwa na Jarida la Afya la TIME anasema kuna aina mbili za maumivu ya matiti; Maumivu yanayotokana na hedhi ya kila mwezi ambayo mwanamke anapata ikiwa ni sehemu ya maumbile ya kibaolojia na yanaweza kutokea kwenye matiti yote mawili.

Aina ya pili ni maumivu ambayo hayatokani na hedhi au mzunguko wa damu ambapo husababishwa na maambukizi au kunyonyesha. Hotokea zaidi kwenye misuli ya kifua ambapo huwaathiri titi moja au yote mawili na wakati mwingine sehemu ndogo tu ya titi.

Zifuatazo ni sababu za kupata maumivu kwenye matiti:

Kupata Hedhi

Robo tatu ya maumivu ya matiti ni matokeo ya kuzalishwa kwa homoni za ‘Estrogen’ na ‘Progesterone’ ambazo hutokea wakati wa hedhi ya kila mwezi.

 “Maumivu ya matiti yanayotokana na homoni yanampata kila mwanamke”, anasema Dkt. Monique. “Haijalishi wana miaka mingapi 14 au 44 kama bado wanapata hedhi wako katika hatari ya kupata maumivu ya matiti”.

 Kwa baadhi ya wanawake, maumivu hayo huondoka yenyewe ndani ya wiki moja hadi siku 10. Wengine hutumia dawa za kutuliza maumivu. Kubadili mlo inaweza inaweza kusaidia kutuliza maumivu yanayotoka na hedhi kwa sehemu ikiwa ni pamoja na ulaji wa mbegu za katani (Flaxseed) na kujiepusha na vyakula vyenye mafuta mengi.

 

Ujauzito

Katika kipindi cha kwanza cha ujauzito, mwili huongeza uzalishaji wa homoni ambazo husababisha mabadiliko ya kimwili ikiwemo kutapika, kizunguzungu, kuchagua vyakula, kichefuchefu na maumivu ya matiti.

 Tishu za matiti huongezeka, maziwa kujaa na chuchu kuimarika, anasema Dkt. Jennifer Wu wa Hospitali ya Lenox Hill iliyopo katika jiji la New York. Maumivu hayo ni kwasababu ya “mabadiliko ya homoni”, anasema ambapo inajumuisha mfumo mpya wa uzalishaji homoni kwa ajili ya kulinda mimba.

 

Unyonyeshaji Watoto

Mdomo wa mtoto ni wa asili kwa mara ya kwaza anapoaanza kunyonya inaweza kusababisha hali isiyo ya kawaida na maumivu kwenye matiti. Hii hutokea kama mtoto hajaweka vizuri mdomo wake kwenye chuchu lakini akizoea maumivu hayo huondoka.

Pia maumivu yanaweza kutokea kama una maambukizi kwenye mfuko wa maziwa. Ukiyataza, “ maziwa yako yanakuwa yamevimba” anasema Dkt Wu. “Yanaweza kuziba na kujaa sana”. Muone daktari ikiwa hali hiyo itaendelea kwa siku kadhaa.

Kufanyiwa Upasuaji

Mstuko (Trauma) wowote kwenye matiti unaweza kusababisha maumivu ikiwemo upasuaji, majeraha, kuondolewa kwa sehemu ya nyama ya mwili na ngono zembe.

Vidonge vya uzazi wa mpango

 Aina yoyote ya dawa ambayo ina homoni za kuzuia mimba zinaweza kusababisha maumivu ya matiti. Muone daktari kama maumivu unayoyapata yamesababishwa na matumizi ya njia za mpango.

Kwa sehemu kubwa maumivu ya matiti hupotea yenyewe na yanaweza kutibika kwa urahisi. Dkt. Monique anashauri kuwa ikiwa maumivu yataendelea kwa wiki moja hadi mbili muone daktari. Anaeleza kuwa unaweza kumuona Daktari kama una dalili zingine ikiwemo kutoka usaha, matiti kuvimba na kuwa mekundu.

tushirikishane
  • Show Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

comment *

  • name *

  • email *

  • website *

Sponsors

tushirikishane

You May Also Like

Is Tanzania’s Adolescent Fertility Rate Three Times Higher Than Global Counterparts?

The Comprehensive Community-Based Rehabilitation in Tanzania (CCBRT), an organization ​which works to provide affordable medical and ...

Zijue faida 11 za kulala uchi au mtupu nyakati za Usiku

UMEZOEA kulala na nguo nyepesi za kulalia? Au unahisi vizuri zaidi ukilala na nguo ...

Vifo vyashamiri kwa wanaotoa mimba Tanzania. Wazanzibari wafanya ngono wakijitambua

WANAWAKE 390,000, kati ya milioni moja, nchini Tanzania hutoa mimba kila mwaka kwa njia ...