Kesi namba 458 inayowakabili Wakurugenzi wa JamiiForums: Mawakili wavutana kuhusu kidhibiti, yaahirishwa hadi Juni 5

MAWAKILI wa upande wa utetezi na wale wa mashtaka katika Kesi namba 458 inayowakabili wakurugenzi wa JamiiForums wamevutana leo kuhusiana kupokelewa kwa kidhibiti mahakamani.

Mvutano huo uliibuka baada ya wakili wa utetezi, Peter Kibatala, kuiomba Mahakama ipokee nakala ya Whois.com baada ya shahidi wa kwanza wa upande wa mashtaka, Habibu Rashid Ntahigie kuikubali, lakini wakili Salum wa upande wa mashtaka akapinga.

Kesi ambayo iko mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Victoria Nongwa, ilifunguliwa na Jeshi la Polisi ambapo washtakiwa Maxence Melo na Mike Mushi ambao ni wakurugenzi wa kampuni ya Jamii Media inayomiliki mitandao wa JamiiForums na FikraPevu wanakabiliwa na mashtaka mawili.

Wakili Salum alisema kwamba, shahidi yuko kizimbani kuwakilisha upande wa mashtaka na kwamba hawajui nakala hiyo ilitolewaje mtandaoni kwa kuwa hata muhuri ni wa Jamii Media ambao hawana mamlaka ya kuidhinisha nakala hiyo.

Hata hivyo, Wakili Kibatala alipinga na kusema hakuona pingamizi la kisheria kwa sababu shahidi ambaye ni mtaalam wa IT ameitambua na hajaikosoa na kwamba ameomba ipokelewe kama ilivyo.

“Sijaona objection (pingamizi) ya kisheria. Shahidi ambaye ni mtaalam wa IT ameitambua na hajaikosoa na ameomba ipokelewe kama ilivyo. Shahidi ni shahidi wa anayoyafahamu na ndiyo maana ameapishwa yeye, kazi ya upande uliomuita ni kumprompt (kumhamaisha) kueleza anayoyafahamu… So hakuna uwakilishi wa shahidi… na hii inaondoa hata objection (pingamizi) iliyowekwa… Mradi shahidi ameiown (ameimiliki) hiyo document (waraka) naomba ipokelewe kama Exhibit PI,” alisema Kibatala.

Upande wa mashtaka umepinga kwa kusema nakala hiyo siyo halisi hivyo ni lazima iidhinishwe.

Kutokana na mvutano huo wa kisheria, Hakimu Nongwa amesema kwa kuwa kuna vifungu wametaja itabidi akavipitie kwani sheria ya ushahidi kwa mambo ya mtandao imebadilika, hivyo atavipitia ili ajue kama ataipokea hiyo document au la.
“Tarehe 5 mwezi wa 6 tutatoa uamuzi na shauri litaendelea… shahidi naomba ufike siku hiyo,” alisema hakimu na kuahirisha kesi hiyo.

Bottom of Form

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, washtakiwa hao wanadaiwa Kuendesha mtandao ambao haujasajiliwa nchini do-tz, yaani .tz (Tanzania domain), na Kushindwa 'kutoa ushirikiano' kwa Jeshi la Polisi kwa kuzuia taarifa binafsi za wateja wa mtandao wake.
Habibu Rashid Ntahigie, ambaye ni shahidi namba moja katika kesyeye ni Meneja wa Rejistry ya .tz. Elimu yake ni shahada ya uzamili ya IT na Management, isipokuwa kitaaluma ni Mhandisi wa Umeme.

Yuko kwenye ajira hiyo tangu 2008 wakati kampuni ilipoanzishwa na ni mwajiriwa namba moja wa kampuni.
Tanzania Network Information Centre (tzNIC) au Rajisi ya dot tz ni kampuni inayoendesha na kusimamia rasilimali ya nchi (dot tz) kwa ajili mawasiliano kupitia mtandao wa Intaneti.

tzNIC inasimamia rasilimali mojawapo ya mawasiliano Tanzania yaani kikoa cha .tz wakati rasilimali nyingine ni +255, ambapo Watanzania wamepewa herufi 2 wazitumie wakati wanatumia mitandao.

Mwenendo mzima wa kesi hiyo leo hii ulikuwa kama ifuatavyo:

Wakili wa Serikali anayeitwa Salum anauliza: Wadau wenu wakubwa ni nani? Au taasisi gani zinatumia hiyo .tz?

Shahidi: Kwa mujibu wa EPOCA imeainishwa kuwa taasisi zote za serikali na binafsi zinasisitizwa/kuhimizwa kutumia .tz

Salum: Dhumuni ni nini?

Shahidi: Kwanza, Identity (utambilisho) kwenye mtandao. Pili, Credibility (kuaminika) kwenye mtandao. Lengo lingine kubwa ni kupunguza gharama za mawasiliano kwenye mtandao.

Salum: Usajili umeanza rasmi lini?

Shahidi: 2009….

Salum: Ukiangalia upande wa pili wa mahakama (upande wa watuhumiwa) kuna unayemfahamu?

Shahidi: Ndio namfahamu Maxence Melo.

Salum: Ulimuona wapi?

Shahidi: Kwenye press conference ya kutangaza kikoa cha .tz New Africa Hotel mwaka 2010.

Salum: Ulifahamu anahusika na nini?

Shahidi: Wakati ule sikujua…ila baadae nilijua kuwa ana mtandao anaendesha. Nafahamu kuwa anaendesha mtandao wa Jamiiforums.com .
Salum: Wamewahi kujisajili kwenu? 

Shahidi: Ndio wamesajili majina mawili, JF.co.tz na jamiiforums.co.tz.

Salum: Unakumbuka walisajili lini?

Shahidi anataka arefresh memory sababu hakumbuki accurately…. (anataka kusoma).
Wakili wa JamiiForums anasema lazima na yeye aone atakachosoma.

Lissu anasema: Hicho atakachosoma ni lazima iwe alikiandika muda huo tukio lilipotokea… hivyo lazima waone asije kuwa kaandaliwa notes.

Wakili wa serikali amewithdraw ombi la shahidi la kurefresh.
Shahidi: Sikumbuki vizuri tarehe lakini ilikuwa 2013, zikisajiliwa miezi tofauti. 2016 zikafutwa miezi tofauti, baada ya kama mwezi mmoja zilisajiliwa tena 2016. Sasa hivi ziko kwenye database, moja ina-expire June mwaka huu nyingine Novemba…

Salum: Kwahiyo sasa hivi ziko mbili kwenye database?

Kibatala: That was a leading Question (Hilo lilikuwa swali la kuongoza).

(Wamevutana kidogo)

Salum: Tuhuma zilizopo mahakamani umezisikia?

Shahidi: Nimesikia kuwa mtuhumiwa hatumii kikoa cha .co.tz.

Salum: Ulichukua hatua gani baada ya kusikia hvyo?

Shahidi: Nilienda kuhakikisha kama wamesajili. Nikakuta ndiyo wamesajili. Ila katika kuhakiki kama wanatumia nimegundua jf.co.tz wala jamiiforums.co.tz hazitumiki. Nimeangalia kama yanatumika kwa barua pepe lakini hayana MS request…hivyo hayatumiki. Hivyo wamesajili lakini hawatumii kwa barua pepe wala tovuti. Kitaalam hiyo inaitwa 'domain parking' yani kuzuia mtu asitumie jina lako.

Salum: Zaidi ya kikoa cha .tz kuna vikoa vingine vinavyotumika kwenye mtandao?

Shahidi: Vipo vingi kama .com ambayo ni generic top level domain. .com inaendeshwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za Marekani, .tz inaendeshwa kwa mujibu wa sheria za Tanzania.

Wakili wa serikali ameuliza swali ila kaambiwa abadilishe aina ya maswali kwani ilikuwa leading question.

Salum: Baada ya kuanzishwa kwa sheria, je vipi kuhusu vikoa vingine?

Shahidi: Sheria haijaongelea vikoa vingine bali imesisitiza tu matumizi ya .tz.

Advocate Peter Kibatala kaingia kufanya cross examination ya shahidi.

Kibatala: Shahidi umesema wewe ni meneja wa tznic?

Shahidi: Ndiyo.

Kibatala: Je, tukitaka kuhakikisha wewe ni meneja utatusaidiaje?

Shahidi: Inabidi umuulize mwajiri wangu.

Kibatala: Kwahiyo hapo uliposimama hatuwezi kujua?

Shahidi: Sijabeba kitambulisho (kaweka mikono mfukoni hakimu kamwambia aitoe).

Kibatala: Kampuni yenu ni registry, je mna register/registers? Yaani mna sehemu ambapo tukitaka kujua huyu kajisajili huyu hajajisajili tunaweza kwenda?

Shahidi: Ndio papo…

Kibatala: Je mahali hapo panaitwaje?

Kibatala: Ukienda kwenye tovuti yetu tznic.org.tz ukurasa wa 1 kabisa ukiweka jina litakupa jibu.

Kibatala: Je, ni nani custodian wa mahali huko?

Shahidi: Kila kikoa kina custodian wake…Pia kama ni mtaalam ukienda kwenye platform ya unix unaweza kuingiza domain name kwenye who is.com.

Kibatala: Kutokana na maelezo yako nimeelewa kuwa hakuna issue ya non-compliance kwa kusajili upande wa jamiiforums, ni kweli?

Shahidi: Ni kweli.

Kibatala anaonesha document: Shahidi naomba utuambie kama hii ndio extract ya who is unayozungumzia.

Shahidi: Ni kweli hii ni extract ya who is…

Kibatala: Inaonesha nini hapo kuhusu jamiiforums?

Shahidi: Inaonesha jina jamiiforums.co.tz limesajiliwa June 2016.

Kibatala: Je hiyo jamiiforums.co.tz kama inavyoonekana hapo imekidhi vigezo vya kisheria vya kiusajili?

Shahidi: Nilishatoa ufafanuzi hapo awali kuwa wamesajili majina mawili…lakini sheria inaongelea kuhusu usajili na utumizi.

Kibatala: Je uko tayari kuikabidhi hii document kwa hakimu(extract ya whois) ili itumike kama kithibitisho cha yale uliyosema?

Shahidi: Sina kipingamizi…ni public info.

Wakili wa serikali: Shahidi yuko kizimbani lakini anatuwakilisha sisi…hii document iko mtandaoni na hatujui imetolewaje huko….hata muhuri ni wa Jamii Media, hawana authority ya kucertify hii document.

Kibatala: Sijaona objection ya kisheria..shahidi ambae ni mtaalamu wa IT ameitambua na hajaikosoa na ameomba ipokelewe kama ilivyo…Shahidi ni shahidi wa anayoyafahamu na ndio maana ameapishwa yeye…kazi ya upande uliomuita ni kumprompt kueleza anayoyafahamu…So hakuna uwakilishi wa shahidi…na hii inaondoa hata objection iliyowekwa… Mradi shahidi ameiown hiyo document naomba ipokelewe kama Exhibit PI.

Upande wa Serikali: Hii document ni copy…original document iko kwenye whois…hii copy lazima iwe certified.

Hakimu kasema kwakuwa kuna vifungu wametaja itabidi akavipitie kwani sheria ya ushahidi kwa mambo ya mtandao imechange hivyo atavipitia ili ajue km ataipokea hyo document au la.

Hakimu: Tarehe 5 mwezi wa 6 tutatoa uamuzi na shauri litaendelea…shahidi naomba ufike siku hiyo.

tushirikishane
  • Show Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

comment *

  • name *

  • email *

  • website *

Sponsors

tushirikishane

You May Also Like

Zitto abariki wanachama kuondoka ACT Wazalendo

Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema  chama chake kitaendelea kuikosoa ...

Waziri akiri maeneo mengi ya taasisi za serikali hayajapimwa, wananchi wanavamia na kujenga makazi

Serikali imezitaka taasisi za umma zinazomiliki ardhi katika maeneo ya wazi kupima na kupata ...

Serikali yadaiwa kuibagua Musoma misaada ya Mafuriko; Kisa kuchagua CHADEMA?

OFISI ya Waziri Kuu kitengo cha Maafa, imetupiwa lawama nzito na wananchi wa Manispaa ...