By -

Hospitali zetu kukosa Dawa: Serikali haiwajali wanyonge, inawagwaya Mafisadi wa Escrow – Zitto

Tatizo la dawa nchini ni kubwa kuliko watu wanavyodhani. Na ni bahati mbaya sana Watanzania wengi wanasahau haraka juu ya namna Serikali ya CCM isivyojali kabisa juu ya Afya na Maisha yao. Kuna wananchi wenzangu wengi wananilaumu kwamba kwa kuwajulisha kuwa Hospitalini hakuna Madawa huku Serikali ikinyamazia Ufisadi wa Mabilioni 850 wa "Akaunti ya Tegeta Escrow"...